upimaji na tathimini
> > y Upimajina Tathmini 1. Tathmini ni nini? Ni utaratibu wa kupima na chukunguza hali halisi kwa lengo la kupata data zitakazo mwezesha mwalimu au mtahini kufanya maamuzi yanayohusu urekebishaji au uboreshaji wa mambo mbalimbali katika elimu. 2. Kutahini ni nini? Ni tendo la kutoa seti ya maswali yenye kiwango na mpangilio unaokubalika ili yajibiwe na mtahiniwa ili kupima kiwango fulani cha elimu alichojifunza. 3. Upimaji wa Kielimu ni nini? Ni tendo la kutafuta ni kwa kiasi gani mwanafunzi amepata maarifa na stadi alizofundishwa kufuatana na malengo ya ufundishaji. 4. Mfiko ni nini? Mfiko ni maksi inayoonesha tofauti kati ya maksi ya juu kabisa na maksi ya chini kabisa katika seti ya maksi za watahiniwa. 5 . Ni Zana zipi za msingi zitumikazo katika upimaji wa haraka za kufundisha na kujifunza? Zana zitumikazo katika upimaji wa haraka za kufundisha na kujifunza ni kama vile; Maswali Mazoezi Majaribio na Miti...