MIFU,O YA SIASA
SIASA N,UTAMADUNI NA UTANDAWAZI
1. KUCHANGANUA
MIFUMO YA SIASA ILIYOPO KATIKA JAMII ILI KUBAINI NA ATAHRI ZAKE.
1. DHANA YA SIASA
Siasa;- ni njia ya kufanya maamuzi
katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa
ya kimatatifa).
Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali
wenye nguvu au mamlaka.
Katika demokrasia
kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya
watu wote kuchangia maamuzi.
2. MIFUMO YA SIASA
Hapa chini, mifumo mingine ya
kisiasa huelezwa kifupi:
Utawala wa
Kifalme
ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka
ya dola na ya serikali Mfalme. Katika mfumo huu madaraka hurithiwa na mtu wa familia ya kifalme.
Utawala wa
Kiimla
ni mfumo wa uongozi unaotoa madaraka
yasiyo na mipaka kwa kiongozi. Katika utawala huu watu binafsi hawana haki na uhuru katika
maamuzi.
Utawala
finyu
ni mfumo unaowapa wachache nguvu za
maamuzi katika dola na serikali. Nafasi ya wachache hawa hutokana na haiba na uwezo wao kiuchumi, kijamii, kijeshi au
kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni
nadra sana siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa makabaila.
Utawala wa
Umma
ni utawala unaotokana na jamii
kuamua misingi ya kujiongoza. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama Utawala wa
Kidemokrasia.
Demokrasia;-
kwa asili neno hili limetokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni demos
linalo maanisha watu na kratos
linalo maanisha nguvu tawala.kwa maana hiyo demokrasia ni utawala aunguvu ya
watu.
Demokrasia ni mfumo unatoa fursa
ya madaraka kwa umma moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa.hivo tunapata
aina mbili kuu;-
- Kuwakilishwaji
- Moja kwa moja(ushirikishwaji wa watu wote)……………….
na
umegawanyika katika sehemu nne.
- Demokrasia Baguzi
ni aina ya
Demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi.
- Demokrasia Duni
ni aina ya
demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu
kuunda serikali mfano: chama - serikali.
- Demokrasia Endelevu
- Demokrasia Shirikishi
katika
aina hii ya Demokrasia wachache hupewa dhamana na wengi katikauwakilishi
wa jamii katika maamuzi.
Wachache
uchaguliwa na wengi kwa njia ya Demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba ya
nchi hiyo. Mfano: Wabunge
uwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya
maendeleo ya nchi.
.Misingi ya demokrasia.
- Usawa
- Uwajibikaji
- Uchaguzi ulio huru na haki
- Uhuru wa kiuchumi
- Utawala wa sheria
- Vyama vingi vya kisiasa
- Haki za binadamu
- Uadilifu.
3.ATHARI ZA MIFUMO YA SIASA KATIKA
JAMII-ULIMWENGUNI.
SWALI;Kuna athari gani zinazoweza kujitokeza kutokana
na
mifumo hii ya siasa katika jamii na
ulimwengu kwa ujumla.
4.DHANA YA DOLA
Dola ( nchi, serikali,
taifa; ing.
state) ni utaratibu wa kisiasa wa jamii katika eneo fulani.
Ufafanuzi wa "Dola"
Fani mbalimbali huwa na maelezo tofauti
kiasi juu ya maana ya dola:
- sheria hufundisha dola kuwa mamlaka ya jamii ya taifa; ina tabia tatu za kimsingi ambazo ni
- eneo la dola,
- taifa au watu wa dola na
- mamlaka ya dola juu ya watu na eneo lake.
- elimu jamii hufundisha kufuatana na Max Weber dola kuwa jumuiya au jamii ambayo ina mamlaka ya kukubalika ya pekee katika eneo fulani; hivyo ni uhusiano wa utawala wa watu juu ya watu unaofuata haki na sharia.
- elimu siasa hufundisha dola kuwa muundo wa mamlaka ya umma kwa ajili ya kuratibu mambo ya umma.
- falsafa hufundisha dola kuwa utekelezaji wa shabaha za kimaadili za kila mtu na jamii kwa pamoja; Hegel alisema dola ni mwendo wa Mungu katika historia; msingi wake ni akili inayotaka kuwa uhalisia.
Aina za Dola
Dola hutokea kwa maumbo mbalimbali kwa mfano jamhuri au ufalme. Dola inaweza kujitegemea kabisa au kuwa sehemu ya shirikisho au muungano kama Muungano wa Madola ya Amerika. Ndani ya maumbo haya kuna njia mbalimbali za kutekeleza mamlaka na kuratibu serikali kwa mfano kwa njia ya demokrasia au udikteta.
Vyombo vya
Dola
Kiini cha
dola ni utekelezaji wa mamlaka katika eneo fulani. Hapo kuna chombo kinachoitwa
serikali chenye mamlaka haya mkononi. Serikali inaangaliwa na taasisi nyingine.
Katika
madola ya kisasa kuna mgawanyo wa madaraka wa dola kwa taasisi mbalimbali:
- bunge huamua juu ya sheria
- serikali inatekeleza sheria
- mahakama zinaangalia utekelezaji na kuamua kama kuna mawazo tofauti
NGUZO
KUU ZA SERIKALI
- serikali
- Mahakama
- Bunge
Vyombo
hivi ni vyombo vya utendaji katika nchi,shughuli hizo ni kutekeleza utoaji wa
haki,mamlaka ya utendaji kutunga sheria
na utekelezaji wa shughuli za umma.na kila chombo hutekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa katiba.
SERIKALIUTAWALA
Ni chombo kinacho tekeleza madaraka
ya utawala na chenye mamlaka kwa mujibu wa katiba,na serikali yetu hufuata
misingi ya kidemokrasia na haki ya jamii.na wananchi ndio wenye mamalaka kamili
na serikali huwajibika kwa wananchi na utekelezaji wa sera na mipango ya
maendeleo ya nchi.
Nguzo
hii huundwa na viogozi mbali mbali,kila
kiongozi huyo huwa na shughuli zake tofauti za endaji katika serikali
|
RAIS
|
||||||||
|
MAKAMU
WA RAIS
|
||||||||
|
BARAZA
LA MAWAZIRI
|
||||||||
|
WIZARA
MBALAMBALI
|
||||||||
|
WATUMISHI
WA SERIKALI
|
||||||||
Soma na Eleza kazi za
viongozi hao katika serikali
MAHAKAMA
Ni chombo cha kutafsiri sheria na kutoa haki kwa raia wote.
mahakama ni muhimili au nguzo kuu ya tatu ya serikali.Mkuu wa muhimili huu ni
jaji mkuu .
Ngazi ya mahakama Tanzania
ni kama zifuatazo:-
|
MAHAKAMA YA RUFAA
|
|
MAHAKAMA
KUU
|
|
MAHAKAMA
YA HAKIMU MKAZI/MKOA
|
|
MAHAKAMA
YA WILAYA
|
|
MAHAKAMA
YA MWANZO
|
Kazi za mahakama
·
kulinda katiba na utawala wa sheria
·
Kulinda haki za raiya kama zilivyoainishwa katika
katiba
·
Kutatua migogoro kati ya viombo vya dora
·
Kutatua migogoro baina ya raia wenyewe kwa wenyewe
na kuwaadhibu wanao vunja sheria.
·
Kutoa uamuzi wa mwisho katika kutafsiri sheria na kutafsiri sehemu za katiba zinazoleta utata.
BUNGE
Ni muhimili mkuu mwingine wa
serikali.bunge huwekwa na watu ili litunge sheria na kusimamia serikali kwa
niaba yao.Rais pia ni sehemu ya bunge.
Aina za wabunge
1. Wabunge 232 waliochaguliwa kwenye majimbo
wanayowakiisha
2. Wabunge 5 kutoka baraza la wawakilishi
Zanzibar
3. Mwanasheria mkuu
4. Wabunge wa viti maalum wanawake 20% ya
wabunge wa majimbo
5. Wabunge wa kuteuliwa na Rais(nafasi 10)
Tanzania Parliament consists of the
following categories of members: (Article 66 of the Constitution)
- Members elected to represent constituencies.
- Women members whose number shall increase progressively starting with twenty per cent of the members named in sub-paragraphs (1), (3) and (4) of this paragraph, to be elected by the political parties that are represented in the National assembly in terms of Article 78 of the Constitution and on the basis of proportional representation amongst those parties.
- Five members elected by the Zanzibar House of Representatives from among its members,
- The Attorney General.
- Not more than ten members appointed by the President
The 2010 general elections produced
the following numbers:
|
|
|
|
|
1.
|
Members elected from the same
number of constituencies.
|
239
|
|
2.
|
Special seats women members.
|
102
|
|
3.
|
Members elected by the Zanzibar House
of Representatives.
|
5
|
|
4.
|
Attorney General.
|
1
|
|
5.
|
Members appointed by the
President.
|
10
|
|
|
Grand Total .
|
357
|
Kazi za bunge
- To pass laws for the good governance.
- To provide, by giving
legislative sanction to taxation and acquisition
of means to carrying out the work of the government. - To scrutinize government policy
and administration, including
proposal for expenditure; and to debate major issues of the day.
Kamati ya bunge
a) Ulinzi na usalama
b) Mambo ya nje
c) Mashirika ya umma
d) Huduma za jamii
e) Kanuni za bunge
f) Katiba na sheria
g) Mazingira n.k
Viongozi wa bunge
- Spika na naibu spika
- Katibu wa bunge
- Waziri mkuu
- Kiongozi wa kambi ya upinzani
NB
Mkuu wa dola (pia: Mkuu wa nchi) wa nchi ni kiongozi
mwenye cheo kikuu. Lakini si lazima ya kwamba mkuu wa dola ana madaraka mengi
sana. Hali inategemea na katiba ya nchi na utaratibu wake wa kisiasa. Pia si lazima ya
kwamba nafasi ya mkuu wa dola inashikwa na mtu mmoja kwa sababu madaraka yake yanaweza
kukabidhiwa pia kwa kamati ya viongozi.
Mkuu wa
Dola katika Jamhuri
Katika mfumo wa jamhuri ya kisasa mkuu wa dola mara nyingi ni rais
aliyechaguliwa na wananchi wote au na bunge.
Kimsingi kuna aina mbili za wakuu wa
dola katika mfumo huu
- rais ni mkuu wa nchi na pia mkuu wa serikali jinsi ilivyo Marekani, Tanzania na pia katika nchi nyingi za Afrika (serikali ya kiraisi).
- rais ni mkuu wa nchi asiyeshughulika mambo ya serikali jinsi ilivyo Ujerumani au Uhindi (serikali ya kibunge) akiwa hasa mwakilishi mkuu wa taifa.
Katika mfumo wa pili rais anaweza
kuwa na madaraka muhimu hasa wakati waziri
mkuu au serikali iko matatani au baada ya uchaguzi. Mara nyingi rais huwa na
kazi ya kumkabidhi kiongozi wa chama kikubwa wajibu wa kuanzisha serikali na
kutafuta kibali cha wabunge. Lakini kama hakuna chama kikubwa baada ya uchaguzi
au ahieleweki kiongozi yupi atafaulu kukusanya wabunge wengi kwa kuunda
serikali kuna nafasi ya rais ya kumteua kiongozi na kumpa nafasi.
Mfumo wa tatu ulipatikana zaidi
katika historia ni kamati kama mkuu wa dola. Siku hizi inapatikana katika Uswisi (viongozi 7 wa serikali wanaobadilishana kila baada ya
mwaka), Bosnia
na Herzegovina (marais 3 kutoka kila dola la
shirikisho wanaobadilishana baada ya miezi 8) na jamhuri ya San Marino (maraisi 2 kwa pamoja wanoitwa "capitani
reggenti"). Umoja wa Ulaya si dola kamili kwa hiyo hakuna mkuu wa dola lakini kuna
uraisi unaoshikwa na serikali za mataifa wanachama yote kwa kubadilishana zamu
za miezi 6.
Katika nchi nyingi rais ana pia
nguvu ya veto juu ya
sheria zilizopitishwa na bunge. Hii ni pamoja na nchi ambako sheria zote au
sheria kadhaa zinapaswa kutiwa saini na rais baada ya kupitishwa na bunge. Rais
akikataa azimio la bungo haiwi sheria. Ama inarudi bungeni au mahakama kuu
inapaswa kutoa azimio.
Mkuu wa
Dola katika Ufalme
Katika nchi
zilizo chini ya muundo wa ufalme (pamoja na emirati, usultani au utemi) mkuu wa dola anaitwa mfalme au sultani n.k.
Hapa kuna pia
viwango vya madaraka kwa mfalme vinavyofanana na nafasi ya rais katika jamhuri.
Katika historia
mara nyingi wafalme walikuwa na madaraka makubwa sana wakiunganisha uongozi wa
serikali pamoja na nafasi ya hakimu mkuu na pia madaraka ya kidini.
Siku hizi kuna
wafalme wachache tu ambao ni watawala wanaoshika madaraka yote ya serikali na
hawabanwi na katiba katika utekelezaji wa utawala wao. Mifano yake ni wafalme
au masultani wa Saudia,
Omani, Qatar, Uswazi, Brunei na Papa kama mkuu wa Dola la Vatikani.
Lakini wafalme
wengi wako chini ya utaratibu wa katiba ya nchi na mara nyingi wana nafasi
inayolingana na rais katika mfumo wa serikali ya kibunge. Katika nchi hizi
sheria na maazimio ya mahakama yanaweza kutangazwa kwa "jina la
mfalme" lakini hali halisi kiongozi mwenye madaraka makubwa ni waziri mkuu
kama kiongozi wa serikali aliyechaguliwa au kuthebitishwa na wabunge wengi.
Katika Ufalme wa Maungano (Uingereza) malkia inatangaza kila mwaka shabaha za
serikali bungeni lakini hali halisi anasoma tu hotuba iliyoandikwa na waziri
mkuu.
Katiba
Katiba ni sheria au kanuni zinazoanisha jinsi
ambavyo nchi, chama, au shirika vitakavyoendesha shuguli zao.
Kwa upande wa nchi, katiba ni sheria mama inayoainisha misingi mikuu ya kisiasa
na kuonyesha madaraka na majukumu ya serikali.
Katiba za nchi pia huanisha haki za msingi za wananchi.
|
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni
mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Katiba kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Kuna aina kuu mbili za Katiba
ambazo ni:
Maoni
Chapisha Maoni