UTANDAWAZI NA UTIMILIFU WA UNABII
(GLOBALIZATION AND THE FULLFILMENT OF THE PROPHECY)
NA. EV.Amos robart Ndaro Zanzibar - Tanzania
MAANA YA UTANDAWAZI
         Utandawazi ni mfumo wa ulimwengu wenye lengo la kuinua uchumi, kwa njia ya biashara na mtiririko wa fedha. Ni shughuli za watu (kazi), maarifa (teknolojia) zinazofanywa bila kujali mipaka ya mataifa, Mfumo huu unavuka mipaka ya tamaduni, siasa na mazingira.
                              AU
         Utandawazi ni mfumo wa utawala, sayansi na teknolojia unaofanya dunia kuwa kijiji kimoja katika biashara, uchumi, mawasiliano n.k. ni hali ya muingiliano wa mataifa mbalimbali katika nyanja mbalimbali.

MALENGO YA UTANDAWAZI
  1. Kuboresha maisha ya watu
  2. Kuondoa umaskini na kuinua uchumi. Inakadiriwa kuwa ifikapo 2015 umaskini utakwisha kwani uchumi wa watu utakua bora zaidi.

MAENEO MANNE YA UTANDAWAZI
BIASHARA-Ushirikiano wa uuzaji bidhaa toka nchi moja hadi nyingine, utasaidia kuinua uchumi na kuleta maendeleo.
UWEKEZAJI WA MITAJI (Capital Investment)-Nchi tajiri na watu wenye uwezo duniani wawekeze mitaji yao katika nchi maskini.
UHURU WA KUSAFIRI-Watu waruhusiwe kutoka nchi moja hadi nchi nyingine kutafuta kazi na maisha bora.
KUENEA KWA MAARIFA (Technology)-Kuboresha mawasiliano na mfumo wa upashanaji habari.


NYANJA ZA UTANDAWAZI
1. Siasa 2.Uchumi 3.Mfumo wa maisha 4.Mazingira   5.Elimu   6.Technology 7.Dini

MITAZAMO YA MATAIFA MBALIMBALI JUU YA UTANDAWAZI
  • Mataifa mengine yanauona utandawazi kama mfumo utakaoleta maendeleo na faida. Yanauona utandawazi kama ufunguo wa maendeleo ya uchumi wa dunia.
  • Mataifa mengine yanauona utandawazi kama mfumo unaolenga kuyanufaisha mataifa machache. Hivyo mataifa yameingiwa na uoga yakiamini kwamba utaondoa usawa kati ya taifa moja na jingine, utasababisha ajira kuwa ngumu na kuleta ugumu wa maisha.
  • Utafiti unaonesha kwamba, tangu mwaka 1980 utandawazi ulipoanza kuvuma, mataifa yaliyojiingiza katika mfumo wa utandawazi yanakua haraka kiuchumi na kupunguza umasikini.
  • Utandawazi ulipoanza kushamiri nchi za Latini Amerika na Afrika zilisita kuingia katika mfumo huu. Uchumi wake ukaanza kudumaa na hatimaye kuporomoka. Umasikini ukaanza kuongezeka na thamani ya fedha ikashuka haraka kwa kiwango cha kutisha. Nchi nyingi za Afrika ziikawa na hali mbaya.
  • Kadiri nchi hizi zilivyokubali kuingia katika utandawazi, mapato yaliongezeka, mabadiliko yakaanza kuonekana, sasa ulimengu umehakikisha kwamba kuruhusu utandawazi ni kuruhusu uchumi kukua, na kuruhusu maendeleo kupatikana ni kuondoa umasikini na ule ufukara wa kupindukia.

VYOMBO VINAVYOSIMAMIA UTANDAWAZI
    1. Matajiri wenye fedha duniani
    2. Wafamasia wakubwa duniani
    3. Familia ya kifalme ya uingereza
    4. Viongozi wa viwanda vikuu duniani. Ambao ni wanachama wa G8 yaani Marekani, Uingeerza, Ujerumani, Italia, Austraria, Newzland n.k.                    Hivi karibuni viongozi wa G8 wamekutana Uingereza baadhi ya agenda zao ilikuwa jinsi ya kukabili ongezeko la joto duniani, maana mionzi ya jua inazidi kuharibu ozone layer na mazingira, kusameha madeni nchi masikini, kusaidia nchi za kiafrika, uchumi n.k
Vyombo hivyo vyote vinacheza mpira mmoja, kuhakikisha utandawazi unapindua dunia yote,

Yeyote anayeonekana kuwa kinyume na wenzake anauwawa. Mifano ya waliouwa ni
  • Raisi kenedy (USA)
  • Admiral Bhotto (Pakistani)
  • Aldo Moro (Italy)
Admiral Borda na William Colby, waliuawa kwa sababu hawakuwa tayari kushirikiana na wenzao na wakaanza kuvujsha siri za agenda za utandawazi nje.


SERA ZA UTANDAWAZI

  1. SIASA
Kuna machafuko mbalimbali ya kisiasa katika dunia

SERA
                    i.            Sera ya kuboresha dunia iwe ni mahali pa amani.
Amani ya ulimwengu haiwezi kupatikana mpaka ulimwengu ungekuwa na serikali moja (a one world government and one unit monetary system in the form of feudal system as it was in the middle ages. The aim is nothing less than to create a world system of financial control in private hands able to determine the political system of each country and economy of the world as a whole)
     Ulimwengu wote uwe na mfumo mmoja wa utawala unaojulikana kama ‘NEW WORLD ORDER’ Maagizo yawe yanatoka kwenye central place especially the U.S.A government. Rev 13;11 Akanena kama joka ( the USA government superpower)
 Mfano wa maagizo yanayotekelezwa ni;
·         Mfumo wa vyama vingi ( multipartism)
·         Ubinafsishaji (privatization)
·         Cost sharing
·         Trade liberalization
                  ii.            Ili kufanya ulimwengu uweze kutawalika  Vizuri na kwa urahisi;
  Nchi zote zigawanyike katika maeneo ya kijiografia kulingana na tamaduni zao.
·         East African Community (EAC)
·         Southern Africa Development Community(SADC)
·         Umoja wa falme za kiarabu
·         European Union(EU)

MALENGO;
    
  1. Ili USA iweze kutawala vizuri
  2. Easy enaction/introduction/announcement of SUNDAY LAW

EAST AFRRICAN COMMUNITY

Achievements;
       I.      Kuimarisha soko la pamoja
    II.      E.A Parliament
 III.      E.A Court
 IV.      E.A Passport

On progress achievements/ Aims
    V.      Kuuunda jeshi la pamoja, ndiyo maana huwa majeshi yanafanya mazoezi ya pamoja.
 VI.      Kuwa na sarafu moja
VII.      Kuwa na utawala mmoja

MATESO YATAKAPOANZA;

  Mahakama zinatengemea ‘Universal law’ ili kuhukumu watu watakaovunja sheria. Universal law zina nguvu kushinda National law.
   Jumapili ikianza watu wa Mungu (wa S.D.A) watahukumiwa na universal law za umoja wa nchi na sio National law.

                iii.            Ulimwengu unakabiliwa na vita vya magaidi waliotapakaa kila nchi.
Mataifa ya watu hayawezi kuboreshwa mpaka matifa yawe na amani. Suala la magaidi haliwezi kuisha mpaka mataifa yaungane na kuwa na nguvu moja.
                iv.            Vyombo vinavyoshughulikia umoja kama vile UN,AU,etc viimarishwe
Liundwe jeshi la Africa, Ulaya n.k ili kulinda amani ya mataifa. Kuundwe mahakama za kiimataifa ili kushughulikia makosa ya waalifu.
                  v.            Sheria zitungwe kwa pamoja.
Ndivyo maana tuna bunge la
·         Afrika mashariki
·         Ulaya
·         Afrika n.k.
All laws will be uniform under a legal system of world court practicing the same unified code of laws, backed by one world government, police force and a one world unified military to enforce laws in all former countries where no national boundaries will exist.
Those who are rebellions will simple be stared to death or be declared out of laws, thus a target for any one who wishes to kill them
                vi.            Kwa kuwa jumapili itafanywa kuwa siku ya pekee ya ibada na mapumziko;
Watunza SABATO watahesabiwa kuwa wavunja sheria za nchi (universal law);hivyo watastahili kuuawa
              vii.            Passport zitengenezwe zinazojumuisha nchi kadhaa pamoja

MSIMAMO WA KANISA LA WAADIVENTISIA WASABATO (SDA) NA MFUMO WA SIASA.
      (Kulingana na Biblia, Roho ya unabii na kanuni za kanisa)

     Tanzania imeingia katika demokrasia ya vyama vingi,kwa hiyo kuna haja ya washiriki na wafanyakazi wa kanisa kufahamu msimamo wa kanisa kama ulivyoelekezwa na Biblia na Roho ya unabii juu ya siasa za vyama na kupiga kura(vote)
     Maana ya neon SIASA; ni kutenda na watu kupingana wao kwa wao.(Dictionary ya Kiswahili uk.84) na kuwafanya wawe na mashaka na uongozi wao ni kujivutia wao.
     Tafuteni kwa bidii  kuwa na amani kwa watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemuona Bwana asipokuwa nao; Waebr.12;14
    Hili ndilo fungu letu kuwa juu ya somo hili.(REF.TO THE ATTACHMENT ...)


2. ELIMU

  1. Sera ya utandawazi inawataka watu wasome.
Mkakati ni kuboresha mashule na kuinua kiwango cha taaluma ya waalimu; ili kupata wasomi watakaosimamia utandawazi.
  1. Kwa sababu ya kafufua uchumi na mwingiliano wa mataifa mbalimbali.
Hali ya maisha itapanda, watakaofaulu kumudu maisha ya Zama za utandawazi Ni watu waliosoma Sana, walio na elimu ndogo wataishi maisha duniani wala hawatajulikana Kama wako duniani.

3. UHURU WA JAMII (COMMUNITY FREEDOM).

  1. Utandawazi unadai uhuru wa watu kutenda jambo bila kuingiliwa na mtu (yaani conscious freedom)
  2. Hakuna kitu kinachoitwa dhambi ila mabadiliko ya jamii(changes in the society)
    • Kuona jinsia moja na mabadiliko ya jamii
    • Boyfriend/girlfriend
    • Kumchapa mtoto ni kumdharirisha
  3. Shetani amesababisha kusambaratisha familia kupitia mfumo wa utandawazi. Familia zikisambaratika hakuna kanisa tena.

4. LUGHA

Sera hii inakazia kuimarisha lugha tatu yaani
a.       Kiingereza
b.      Kiswahili
c.       Kafaransa

5. DINI
Utandawazi unapendekeza kuwepo na DINI moja ya ulimwengu na siku moja ya IBADA
·         Universal Religion/universal day of worship
·         Dini hiyo ni Romani Catholic(RC)
·         Siku ya ibada ni jumapili

BARUA YA KIKATOLIKI ILIYOANDIKWA NA PAPA PIUS WA KUMI NA MOJA (11) (REF.TO ATTACHMET……..)

6 SAYANSI NA TEKNOLOJIA

  1. Sera ya utandawaza itahakikisha kuwa sayansi na teknolojia inapenya kila mahali. Hili litasaidia kufanya ulimwengu uwe kijiji kimoja. Television, simu, computer, internate, satellite n.k. zitapelakwa kila mahali ili kuboresha mawasiliano. Ndiyo maana baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania imewafanya walio na simu za mkononi kusajili LINE ZAO ZA SIMU na simu zao.
  2. Sera hii itarahisisha mawasiliano katika tangazo la Jumapili.
Daniel 12; 4 maarifa yataongezeka.

7. MFUMO WA MAISHA (LIFE STYLE)

Sera ya utandawazi inakubali mfumo wa maisha wa nchi za magharibi kuwa ndio mfumo unaopaswa kukubalika/kuenea katika nchi zote.
 Hali ya maisha ya watu iinuliwe kufikia kiwango cha nchi za magharibi. Tufanane nao hata mfumo wa maisha yao ya aibu. Mfano mavazi ya nusu uchi, yanayobana na yasiyo na hashima. Mwanzo 3; 7; 21.
  Ulimwengu unapaswa kufuata tamaduni za nchi za magharibi katika,
·         Mavazi
·         Chakula
·         Mahusiano
·         Malezi ya watoto
·         Muziki n.k

SIFA ZA MAVAZI

(From Roho ya Unabii- kitabu cha Child Guidance pg 413_415 na Kutafanyika Njia pg 204)
  1. Yaoneshe Elezo la hali ya mwanamume/mke
    • Dewtronomy 22;5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume (vice versa) ni chukizo kwa bwana
    • I Wakorintho 14;40 mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu
  2. Yasiwe na mapambo/madoido mengi
  3. Yapatane na kanuni za Neon la Mungu. Mithali 7;10

Mavazi yanayobana, nusu uchi, yanayoangaza yote ni ya kikahaba yanavuta watu kufanya ngono.
  1. Yapatane na kanuni za kiafya. Ambayo yanaingiza hewa kwa uzuri kabisa
  2. Yawe ya kusitiri mwili
MAVAZI NA MAPAMBO

Muonekano wa nje ni ishara kuonyesha jinsi moyo wa matu ulivyo(IT 136) kama sisi tu Wakristo tunamfuata Kristo, hata endapo njia tupaswayo kupitia Hupingana na mielekeo yetu ya asili:-
·         Hamna manufaa yoyote kuwaambia imewapasa kutovaa ama kile,kwa maana kama moyo unavutiwa na vitu kama hivyo visivyofaa kuachana na mapambo hayo kutakuwa kama mkataji wa matawi ya mti.jambo ambalo siyo ufumbuzi wa kudumu yatachipua baadae. Yatupasa kujenga Dhamiri safi kuanzia moyoni ili ilete ufumbuzi wa kudumu wa kutoyataka mapambo hayo tena.
·         Tuenende kwa uangalifu na hadhari mbele za Mungu. Kwa kufuata desturi za kuvaa mavazi yale yanayopelekana na kanuni za kiafya na neon la Mungu.
·         Dada zetu wanapaswa kuvaa Kwa wepesi mavazi ya kawaida tu. Mavazi ya kujisitiri, ya heshima na adabu pamoja na utulivu.
·         Toa kwa ulimwengu kielelezo kilicho hai cha kujipamba kwa ndani kwa pambo la Neema ya Mungu.(3SM 242)


SERA ZA UTANDAWAZI KWENYE MFUMO WA MAISHA

Ili tamaduni zao (nchi za magharibi) zitawale maisha yetu;
                    i.            Program nyingi za T.V ni za nchi za Magharibi.

TELEVISHENI NA MAJUMBA YA TAMASHA
Miongoni mwa mahalii pa hatari sana patembelewapo na watu kwa ajili ya starehe ni majumba ya tamasha na sinema. Ndipo mahali penye maovu mengi hasa, ambapo tabia mbaya na mielekezo ya dhambi vinaimarishwa na kuthibitishwa kwa;
  1. Kuangalia na kusikiliza nyimbo za kishenzi,miondoko ya kihuni inayochochea tama za mwili, maovu na kuhafifsha hali ya uadilifu
  2. Kila kijana  ambaye ana mazoea ya kuhudhuria maonesho kama hayo ataharibiwa kimaadili kwa;
    • Kuharibu mawazo yaliyo na mwelekezo wa dini kutia sumu fikira
    • Kupunguza nguvu ya kupenda furaha na utulivu na taratibu halisi za maisha
    • Tamaa za vinywaji vyenye kulevya inaongezeka

                  ii.            Internet, novel zote ni za nchi za magharibi
                iii.             
                iv.            Hata rangi yetu wanataka tuikatae; ifanane na nchi za nje. Hii ndo maana maduka mengi yamejazwa na COSMETICS

WITO; E.G WHITE- maintain your Natural beauty.
                  v.            Maadili ya nchi za magharibi  upande wa malezi ya watoto, watoto hawatakiwi kuadhibiwa kwa fimbo
Biblia inasemaje? Mithali 22; 15, 23; 13-14

                                                     MALEZI YA WATOTO
UMUHIMU WA IBADA YA FAMILIA;
  1. Kuungama na watoto (AYUBU    ), jioni na asubuhi ungama na watoto wako katika kumwabudu Mungu mkisoma neno lake na kuimba sifa zake.
  2. Sifa kwa mama waaminifu;
Wengi watainua taji zao za utukufu na kusoma kwa mama zao wakisema kwa neema ya Mungu mama huyu alinifanya mimi jinsi nilivyo, mafuundisho yake, maombi yake yamepata kuwa Baraka kwa mkono wangu wa milele.Malaika wa Mungu huyapa sifa za milele majina ya wamama ambao juhudi zao zimewaleta watoto wao kwa YESU.(CE-668)

SIFA ZA IBADA YA FAMILIA
  1. Iwe fupi na Changamfu
 
 Msiwaache watoto au mshiriki yeyote wa familia yenu kuyahofu kwa sababu yanachosha au kukosa mvuto.

  1. Somo la kueleweka
  2. Kifungu cha maandiko kiwe kinachovutia na kinachofahamika kwa urahisi
Mafungu machache yanatosha kulipamba somo ambalo laweza kujifunzia na kuwekwa katika matendo wakati wote wa usiku.
  1. Iwe na nafasi ya maswali, nyongeza au kisa vinavyofanya somo lieleweke kwa urahisi na la kukumbukwa


                vi.            Vijana waachiwe huru i.e conscious freedom
Vijana waruhusiwe kufanya mapenzi kuwa na boyfriend na girlfriend.
              vii.            Trial marriages
            viii.            Ndoa za ushoga, mume na mume, mke na mke
Utandawzi unafanya dunia kuwa kama Sodoma na Gomora, Warumi;24-27, Mathayo 24;38-39

Maana ya Sodoma ni kitendo cha mtu jinsia saw kumuingilia mwenzake wanaofanana jinsia na maumbile

8. UCHUMI
Hali ya uchumi ni mbaya na mtikisiko wa uchumi uliikuumba dunia yote
SERA; ili kuinua uchumi/maisha ya watu toka katika hali duni;
  • Ni lazima ucumi ushikwe na nchi tajiri au makampuni yenye uwezo
  • Nchi tajiri ziruhusiwe kuwekeza katika nchi masikini kwa mashariti nafuu na mazingira bora ya utekelezaji.
Sera ya ubinafsishaji itumike
Wawekezaji waruhusiwe kuwekeza katika nchi masikini
  • Nchi masikini ziruhusiwe kwenda kujinadi nchi za nje. Ndio maana Mh Jakaya Kikwete anakuwa na ziara nyingi nchi za nje
  • Mfumo wa soko HURIA umarishwe.
Nchi zisiwe na mipaka katika kuuza bidhaa zake, mfano ni maonesho ya biashara ya kimataif ya DSM.
  • Uchumi unazidi kuharibika/kuporomoka kwasababu nchi nyingi zimeshindwa kudhibiti USHURU

SERA;
  1. Wawekezaji waruhusiwe kuanzisha vituo maalumu vya biashara yaani TRADE CENTRES ili kuthibiti ushuru, mfano machinga complex, mlimani city, supermarket, plaza. Kuanzisha maduka ya jumla lango ni kuua biashara ndogondogo.
  2. Fedha zote zitunzwe kwenye BANKS. Kuanzisha mfumo wa kununua kwa njia ya kadi (ATM-card system) ili kupunguza kiasi cha watu kutembea na fedha.
All banks to be computerized in order to monitor the money, later on to buy products you must have such cards. Sheria ya kutokuuza na kununua itapitishwa kwa sera hii. Ufunuo 13; 17 no buy or sell until you accept Sunday law.

MATUMIZI YA PESA KUFUTWA IFIKAPO MWAKA 2012(Gazeti la INDEPENDENT LA LODON-UK na Gazeti la NYAKATI la SEPTEMBER 23-29, 2007)
Mr.Peter Ayliffe, ni Mtendaji Mkuu wa taasisi iitwayo VISA EUROPE, iliyopewa kaz ya kusimamia uundwaji wa Teknolojia mbadala itakayochukua nafas ya mfumo wa fedha unaotumika sasa ifikapo mwaka 2012, anasema……………………….MAHALI PA SALAMA, NA WANADAMU WOTE WAKIABUDU DINI MOJA.
      Akiutambulisha mpango huo alisema kuwa kila kitu kimekamilika, majaribio ya awali yamekwisha fanyika na kuonesha ufanisi mkubwa, ambapo kazi inayofanyika sasa ni kukamilisha ubandikaji wa vifaa muhimu kila mahali duniani.
     Ni jambo la kuvutia kwa kuwa matumizi ya mabunda ya pesa au sarafu, zilizokuwa zikitumika tangu enzi za utawala wa RUMI yamefika mwisho, binadamu atarudia ustaarabu wake, hatalazimika kusafiri na mizigo na hofu ya kuibiwa.
      Ubaya wa mfumo wa sasa wa matumizi ya fedha ni kwamba unasaidia kuficha majambazi na magaidi yanayoutesa ulimwengu kupita kiasi.
     Uzuri wa mfumo mpya utapunguzia mataifa duniani gharama kubwa ya kujenga magereza na matumizi ya polisi, kwa kuwa mfumo wenyewe utaweza kudhibiti wahalifu na kuwanyima maficho.
    ‘Ikiwa kundi au mtu ataonekana kuwa ni mhalifu itakuwa rahisi kumdhibiti kwa kuwa takwimu za wanadamu wote wanaouza na kununua zitakuwepo., akionekana kuwa tishio atadhibitiwa na mfumo wa fedha.
    Hata hivyo baadhi ya wanatheilojia wanautazama mpango huo kama moja ya njia muhimu za kutiisha ulimwengu na kuuweka chini ya utawala mmoja na kuabudu dini moja.
     Profesa NEELY HUMPHREY, Mtaalamu wa Theolojia na mchambuzi wa maswala ya dini barani UlAYA anaonya kuwa mpango wa dunia isiyotumia fedha ina lengo moja tu la kuwafanya wanadamu kuwa kama kondoo waliopo chini ya mchungaji mmoja mwenye kushika kamba iliyowafunga shingoni.
      Hii itamaanisha kuwa uhuru wa mwanadamu alio nao sasa wa kujiamulia mambo yake mwenyewe, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kumwabudu MUNGU utakuwa chini ya wanamtandao, hao ndio watakaoamua mtu aende wapi au aishije kwakuwa ndio wanaoratibu maisha yake.Wakiamua mtu asiyekubali wanachotaka asile wala kusafiri hakika hatafanya hivyo.
    Anasema kuwa mfumo huo utaanzia ulaya na utasambaa dunia nzima na harakati za kuundwa kwa mfumo mmoja wa dini duniani ni harakati zilizoanza muda mrefu ,mwanzoni zilikuwa ni za kidini zaidi zikakua na kuwa za kidiplomasia na kisiasa,lakini sasa zimekuwa za  kiuchumi na hapa ndipo penye hatari zaidi.

Uchumi unaporomoka kwa kuwa na sikukuu nyingi za kupumzika.

SERA
  • Zipunguzwe zibaki za muhimu tu
Mapendekezo ya sera hii ya uchumi ni kwamba siku za ibada na mapumziko zipunguzwe ili watu wawe na muda mwingi wa kufanya kazi. Iwepo siku moja ya official day i.e Sunday for resting and worship other days not official

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

upimaji na tathimini

MIFU,O YA SIASA

jipatie tablets,pc.i pad kwa bei ya punguzo zaidi

mapendezo ya utafiti

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA