mapendezo ya utafiti


    PENDEKE  ZO  LA UTAFITI
                  
                    UMRI WA KUANZA ELIMUMSINGI KATIKA KATA YA KIGAMBONI
                                                             DAR ES SALAAM

YALIYOMO
1.SURA YA KWANZA…………………………………………………………………….
1.0 UTANGULIZI…………………………………………………………………………..
1.2 Usuli……………………………………………………………………………………..
1.3 Malengo ya utafiti……………………………………………………………………….
1.3.1 Lengo kuu……………………………………………………………………………..
1.3.2 Malengo mahususi……………………………………………………………………
1.4 Maswali ya utafiti……………………………………………………………………….
1.5 Umuhimu wa utafiti……………………………………………………………………..
2. SURA YA PILI……………………………………………………………………………
2.0 Maandiko ya mapitio……………………………………………………………………..
2.1 Sera ya Kenya…………………………………………………………………………….
2.2 Sera ya Uganda…………………………………………………………………………..
2.3 Sera ya Zanzibar…………………………………………………………………………
2.4 Sera ya Tanzania………………………………………………………………………….
2.4.1 Sera ya elimu mwaka 1995……………………………………………………………..
2.4.2 Sera ya elimu mwaka 2014……………………………………………………………
3 SURA YA TATU………………………………………………………………………..
3.0 Mbinu za utafiti………………………………………………………………………..
3.1 Mawanda(eneo) la utafiti………………………………………………………………
3.2 Walengwa wa utafiti……………………………………………………………………
3.3 Sampuli…………………………………………………………………………………
3.3.1 Usampulishaji………………………………………………………………………..
3.3.1.1 Sampuli lengwa…………………………………………………………………..
3.3.1.2 Sampuli nasibu…………………………………………………………………..
3.4 Njia za kusaili………………………………………………………………………..
3.4.1 Hojaji………………………………………………………………………………
3.5 Maadili ya utafiti……………………………………………………………………..
3.6 Ratiba ya utekelezaji………………………………………………………………....
3.7 Bajeti ya utekelezaji…………………………………………………………………

 1.0 SURA YA KWANZA
                                  
                                  1.1 UTANGULIZI
Kulingana na Sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 1995 inasema Umri wa elimumsingi utakuwa ni miaka saba  na muda wa mafunzo katika elimumsingi utakuwa ni miaka saba,
Vilevile kwa mujibu wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inasema umri wa elimumsingi utakuwa ni kuanzia miaka mine hadi sita na muda wa mafunzo utakuwa ni miaka 10.

  1.2 USULI
Katika sera ya elimu ya mwaka 1995 mwanafunzi alipaswa kuanza shule akiwa na umri wa miaka saba na muda wa mafunzo ulitolewa kwa miaka saba na hii ndio ilikuwa elimumsingi ambayo ilianzia darasa la kwanza hadi darasa la saba(I-VII).
Vilevile kwa mujibu wa sera ya elimu ya mwaka 2014 Wizara ya elimu ikaona ni vyema kupunguzwa kwa umri wa kuanza shule na muda wa mafunzo hivyo ikaweka utaratibu kwamba mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka minne hadi sita (4-6) na elimumsingi itakuwa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne na kutolewa kwa muda wa miaka kumi.Lengo la serikali ni kupata rasilimali watu wenye ujuzi na maarifa kwa muda mfupi watakaoweza kuhimili ushindani wa nchi yetu na nyingine.
Hivyo basi utafiti huu umejikita kuangalia utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014


 1.3 MALENGO YA UTAFITI
1.3.1 LENGO KUU
Kujua utekelezaji wa umri wa elimsingi katika kata ya kigamboni
  
 1.3.2 MALENGO MAHUSUSI
1.Kuangalia ufahamu wa sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014
2.Kuchunguza wanafunzi walioandikishwa shuleni wenye umri wa miaka minne hadi sita(4-6)


      1.4 MASWALI YA UTAFITI
1.Je walimu wana ufahamu juu ya sera ya elimu ya mwaka 2014
2. Kuna wanafunzi wangapi walioandikishwa wenye umri wa miaka (4-6)

1.5 UMUHIMU WA UTAFITI
Utafiti huu utasaidia kutambua kama utekelezaji umefanyika katika umri wa kuandikishwa .
Vilevile utafiti huu unakusudia kujua utekelezaji wa umri wa elimumsingi katika kata ya kigamboni.

 SURA YA PILI
                                       MAPITIO YA MAANDIKO
SERA YA ELIMU YA KENYA
 Kulingana na  sera ya elimu ya kenyaElimu ya msingi Kenya inaanza kwa watoto wenye miaka mitano hadi saba(5-7) baada ya mwaka mmoja wa darasa la awali,mwaka wa kwanza katika shule ya msingi unaitwa darasa la kwanza ambapo shule ya msingi mwanafunzi atahitimu kwa miaka minane(8)
Mfumo wa elimu wa Kenya utakuwa 8-4-4 yaani miaka 8 elimu ya msingi,miaka minne(4) elimu ya sekondari na miaka minne 94) kuhitimu mafunzo,mtaala huu unaondoa mfumo wa elimu wa mwaka 1985 unaosema 7-4-2

SERA YA ELIMU UGANDA
Kulingana na mfumo wa elimu wa Uganda muundo wake ni 27+4+2+3++ ambapo darasa la awali wataanza wakiwa na miaka (3-6) wakati mafunzo ya awali huchukua muda wa miaka miwili ,elimu ya msingi wataanza wakiwa na umri wa miaka saba na mafunzo yatatolewa kwa muda wa miaka saba wakati elimu ya sekondari ya kawaida kuchukua miaka minne,sekondari ya juu miaka miwili na elimu ya juu kuendeshwa kwa kipindi cha miaka (3-5).

SERA YA ELIMU ZANZIBAR
Kulingana na sera ya elimu na mafunzo ya amali(2006) Ina sema kuanza skuli katika umri mdogo ni muhimu kujenga msingi imara wa mafanikio katika kujifunza,sera imeona kuwa umri wa miaka 4-6 ndio muda mzuri wa watoto kujifunza na kufundishika,sera iliyopo inamtaka motto kuanza skuli katika elimumsingi kuwa na umri wa miaka saba hali hii imepelekea wanafunzi wengi kumaliza elimu ya lazima wakiwa na umri wa miaka 16 au zaidi
Vilevile umri wa kuanza elimu ya maandalizi ni miaka minne,elimumsingi miaka sita ,elimu ya sekondari ya awali ni miaka miwili na elimu ya sekondari ya juu miaka miwili na kupelekea kuwepo kwa mfumo rasmi ambao ni 2-6-4-2-3 kwa elimu ya maandalizi miaka miwili,elimu ya msingi miaka 6 ,elimu ya sekondari mpaka kidato cha sita miaka miwili na elimu ya juu itakuwa kwa uchache miaka mitatu.

 SERA YA ELIMU YA TANZANIA
SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 1995
Kwa mujiubu wa sera ya na mafunzo ya mwaka 1995 muundo wa elimu rasmi ulikuwa 2-7-4-2-3++ yaani miaka miwili ya elimu ya awali ,miaka saba ya elimu ya msingi ,miaka minne sekondari ngazi ya kawaida ,sekondari ngazi ya juu miaka 2 na kiwango cha miaka isiyopungua miaka 3 ya elimu ya chuo kikuu vilevile sera hii ya elimu ya mwaka 1995 inaeleza kuwa elimu ya awali ilikuwa inaendeshwa kwa kwa miaka miwili kwa wanafunzi wenye umri wa kuanzia miaka (5-6) na kuweka bayana elimumsingi kuendeshwa kwa miaka saba ambapo wanafunzi walianza shule wakiwa na umri wa miaka saba.

SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA(2014)
Kwa mujibu wa sera ya elimu ya mwaka 2014 mfumo wa elimu rasmi ni 1+6+4+2+3++ ambapo elimu ya awali kutolewa kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 3-5 na kutolewa kwa mwaka mmoja ,elimu ya msingi itahusisha wanafunzi wenye miaka 4-6 na kutolewa kwa kipindi cha miaka sita,elimu ya sekondari ya kawaida itakuwa miaka minne,elimu ya sekondari ya juu miaka miwili wakati elimu ya juu kuchukua miaka mitatu na kuendelea
Kwa mujibu wa sera ya elimu ya mwaka 2014 elimumsingi itatolewa kwa kipindi cha miaka 10 ikiwa miaka sita ni ya elimu ya msingi na miaka minne ya elimu ya sekondari ya kawaida
Hivyo umri wa kuanza shule katika darasa la kwanza kwenye nchi zetu za Afrika mashariki hautofautiani sana kwani Tanzania umri wa kuanza darasa la kwanza ni miaka 4-6,Uganda ni miaka 7,Kenya miaka 5-7,wakati Zanzibar ni miaka 7

                                      SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
Kigamboni ni jina la wilaya katika mkoa wa Dar es salaam Tanzania yenye postikodi namba 17000 kwa mujibu wa sense iliyofanyika mwaka 2012 katika kata ya kigamboni  ina wakazi wapatao 30,496 waishio humo .Kigamboni ina umbo la rasi katika bahari ya hindi na maji ya bandari yametengwa na jiji la Dar es salaam kwa maji ya kurasini creek vilevile kiasili sehemu hii ilikuwa kijiji cha wavuvi.Ktika kata ya kigamboni mawasiliano yapo katika njia ya feri kati ya kigamboni na kivukoni upande wa jiji na barabara ambayo ni ndefu  yenye zaidi ya kilomita hamsini(50)
ENEO LA UTAFITI(Shule)
Watafiti watafanya utafiti wao katika shule za msingi Kigamboni,Ufukoni na Raha leo,utafiti huo utahusu kutaka kujua utekelezaji wa umri wa kuanza elimumsingi kama ambavyo umeelekezwa katika sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014
WALENGWA
Utafiti huu utakuwa na jumla ya watafitiwa (sampuli) yaani kila shule wanafunzi 20,kwa kwa kila shule zitakazofanyiwa utafiti na walimu 7 kwa kila shule zitakazofanyiwa utafiti .mfano

Shule

Walimu(idadi)

Wanafunzi(idadi)

Jumla
Uukoni
7
20
27
Raha leo
7
20
27
Kigamboni
7
20
27
Jumla
21
60
81




                                  USAMPULISHAJI
SAMPULI LENGWA
Watafiti watatumia sampuli lengwa ambayo itajumuisha mwalimu mkuu mmoja(1) kila shule na walimu wa madarasa yaani darasa la kwanza mpaka darasa la nne watakuwa walimu wane(4)

NASIBU
Kupata idadi ya wanafunzi 20(Sampuli) kila shule watafiti watatumia daftari la mahudhurio,baada ya kutambua idadi ya wanafunzi katika darasa husika,watafiti watagawanya idadi  ya wanafunzi 20 ambayo ndio sampuli kasha kila baada ya mwanafunzi namba 20 atachukuliwa kama sampuli.
Vilevile walimu wawili ambao hawakuingia kwenye utafiti kwa wadhifa wao  watafiti wataandika namba katika vikaratasi kulingana na idadi ya walimu waliopo baadae watafiti watavichanganya sana na watafiti watachukua namba 1-2 ya walimu waliookota vikaratasi kasha watafiti watatumia wale ambao wameonekana katika namba husika walizohitaji watafiti.
NJIA ZA KUKUSANYA DATA
HOJAJI/USAILI
Watafiti watatumia njia ya hojaji(usaili) katika  kukusaya taarifa kutoka kwa sampuli ya utafiti inayokusudiwa ,hojaji hii itagawanyika katika sehemu kuu mbili yaani hojaji itakayo fanyika kwa walimu na hojaji itakayofanyika kwa wanafunzi.

MAADILI YA UTAFITI
Kulingana na  basiliana emidu(2018) ameainisha  maadili ya utafiti ambayo ni kama ifuatavyo
·         Hakuna mtu anayelazimishwa kushiriki katika utafiti
·         Watafiti ni lazima waelewe lugha za mwili
·         Ni lazima kuwe na msimamizi mkuu
·         Watafiti ni lazima watambue na waheshimu kuwa kila mtu ana haki ya kupata faragha
·         Kuhifadhi kwa usalama taarifa binafsi
·         Kuheshimu sayansi ya utafiti.

Kulingana na maadili hayo utafiti huu utakuwa na maadili kama ifuatavyo
·         Watafiti lazima wawe na kibal
·         Watafiti lazima wawe na zana zote za kukusanyia data
·         Kuwasiliana na shule zinazo enda kufanyiwa utafiti
·         Watafiti watapaswa kuvaa mavazi yenye haiba nzuri
·         Watafiti watapaswa kujitambulisha pindi wafikapo katika eneo la utafiti
·         Watafiti watapaswa kueleza lengo la uwepo wao katika tafiti
·         Watafiti watapaswa kumvumilia kila mtu na majibu yake.









                      RATIBA YA UTEKELEZAJI

 Shughuli

MEI

JUNI
Tarehe


















Kuandaa vifaa



















Kukusanya data



















Kuchambua data



















Kuunganisha data



















Kuandika ripoti





















                           
                         BAJETI YA UTEKELEZAJI
                                 Makadilio ya gharama
1.Usafiri watu 6@sh5000=3000 kwa siku 2 jumla Tsh 6000/=
2.Chakula watu 6@2000=12000 kwasiku 2 jumla Tsh 24000
3.Vifaa=10000/=
4.Uchapaji na kukamilisha kazi=2000
5.Mawasiliano=2000/=                                                                                                                              JUMLA SH 47000/=
                     

                            MASWALI YA UTAFITI
                   FOMU YA USAILI KWA WALIMU
1.Jina la shule…………………………………………………
2.Mahali ilipo…………………………………………
3.Jinsia
Mwanamme                                         
Mwanamke                           
4.Ulishawahi kuiona sera?
Ndiyo
Hapana
5.Kama jibu ndiyo sera hio ni ya mwaka gani?..............................
6.Wanafunzi walioandikishwa mwaka 2015-2018 ni wangapi?......................
7.Je wanafunzi wenye miaka minne(4) ni wa ngapi?................................
8. Je wanafunzi wenye miaka mitano(5) ni wa ngapi?................................
9. Je wanafunzi wenye miaka sita(6) ni wa ngapi?................................
10. Je wanafunzi wenye miaka saba(7) ni wa ngapi?................................

  



   FOMU YA USAILI KWA WANAFUNZI
1.Jina la shule…………………………………………………
2.Mahali ilipo…………………………………………
3.Jinsia
Mvulana                                         
Msichana
4.Una miaka mingapi?.............................
5.Uko darasa la ngapi?…………………
6.Unajua kusoma?
Ndiyo
Hapana                  
7.Unaweza kuhesabu?        
Ndiyo
Hapana                  
8.Je unajua kuandika?
Ndiyo
Hapana                  




REJEA
Hakielimu(2017),Matokeo ya utekelezaji wa sera ya elimu bila ada kwa elimumsingi nchiniTanzania,utafiti wa kitakwimu;Dar es salaam.
WEU(2005),Mpango wa mafunzo ya walimu kazini daraja laIIIC/B-IIIAupimaji,tathimini na utafiti wa kielimu;Dar es salaam
WEU(1995),Sera ya elimu na mafunzo;Dar es salaam
WEMU(2014), Sera ya elimu na mafunzo;Dar es salaam
https;//www.slideshare.net/ojijop/review-of-education-policy-in Uganda
https;//ww.nuffic.nl>find-a-publication
fortuneof af Africa.com/ug/education-system-in-uganda/
n.m.wikipedia.org/wiki/education-in-kenya



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

upimaji na tathimini

MIFU,O YA SIASA

jipatie tablets,pc.i pad kwa bei ya punguzo zaidi

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA